Justin Kasholo kutoka Bukavu

Wakuu wa mashirika ya kimaeneo ya tarafa yanayojitegemea katika jimbo la Kivu Kusini walishiriki mafunzo kuhusu utawala wa ndani, uundaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya ndani. Shughuli hiyo ilifanyika katika Kituo cha RIO kilicho pa  Nguba kuanzia tarehe moja hadi tatu Desemba  mwaka tunao, chini ya usimamizi wa Wizara ya Mipango, kwa msaada wa kifedha wa Shirika la Ushirikiano la Ujerumani GIZ. Mkuu wa ofisi ya Mpango jimboni, Justin Kasholo ndiye mgeni anazungumza na Jean Kasami. /sites/default/files/2022-12/07122022-p-s-invite_justinkasholocdpansudkivu-00.mp3