Balume Pierre: Masisi wakaaji wanaishi hali mbaya sana

Katika tarafa la Maisisi, wakazi wanaishi hali ngumu sana. Haya ni maoni ya kiongozi wa shirika lisilo la kiserikali la maendeleo ambaye alirejea kutoka eneo hilo. Huyu ni Pierre Balume, mratibu wa Shughuli za Kibinadamu kwa ajili ya uimarishaji wa amani na maendeleo jumuishi, AHCOPEDI, ambaye ndiye mgeni wetu wa siku ya leo. Kulingana naye, raia wanaishi chini ya sheria ya waasi na vile vile vikundi vilivyojihami silaha vya Wazalendo ambao wanaweka sheria kulingana na eneo lao la udhibiti. Kwa upande wa kiuchumi, kuna kushuka kwa bei ya bidhaa za chakula zinazozalimwa pahali, wakati bidhaa za viwandani zinakabiliwa na ongezeko la bei. Pierre Balume anaelezea hali ilivyo hapa katika mahojiano haya na Sifa Maguru…

/sites/default/files/2024-11/061124-p-s-invitegomabalumepierre-00-web.mp3