Kuendelea kwa waasi wa M23 ndani ya tarafa la Walikale kuna athari mbaya kwa uzoefu wa kila siku wa wanafunzi wazaliwa wa tarafa la Walikale huko Kivu Kaskazini, wanaoishi Bukavu jimboni Kivu Kusini. Kiongozi wa chama chao anatoa wito kwa serikali kuzuia njia kwa waasi, ili kuruhusu familia kufanya biashara zao kwa uhuru na hivyo kupata uwezekano wa kukidhi mahitaji ya wategemezi wao wanaosoma Bukavu, kilomita mia mbili makumi tano kaskazini mwa jiji. Espoir BUTERA Jean, mwanafunzi kunako ISP Bukavu, wakati huo huo ni mkuu wa chama cha wanafunzi wazaliwa wa Walikale wanaoishi Bukavu. Yeye ndiye Mgeni wetu, anazungumza hapa kwenye maikrofoni ya Jean Kasami.
/sites/default/files/2024-11/291124-p-sinvitebukabuespoirbuterajeanisp-00-web.mp3