Nasson Murara : Mjini Beni kumekuwa wizi ambao wanatumia mitandao kwa kuiba watu

Katika jiji la Beni, askar polisi kumi, wakiwemo sita kutoka jiji hilo na wanne kutoka tarafa la Beni, wamepewa vifaa na mbinu za kimsingi za uchunguzi wa kidijitali. Mafunzo haya ya siku tano yaliyoanzishwa na kitengo cha polisi cha MONUSCO-UNPOL yanalenga kuwapa maafisa hawa wa kutekeleza sheria ujuzi unaohitajika ambao unaweza kuwasaidia kuchunguza matukio ya kidijitali. Tunazungumza juu yake na Nasson Murara, afisa mawasiliano wa polisi katika jiji la Beni katika mahojiano haya na Marc Maro Fimbo.

/sites/default/files/2025-01/230125-p-s-invitebeninassonmurarapnc-00-web.mp3