Katika tarafa la Beni, sauti zinapazwa kukashifu uchakavu wa mhimili wa barabara ya Eringeti-Kainama. Barabara hii muhimu sana inawezesha usafirishaji wa bidhaa za kilimo na pia inaunganisha Kivu Kaskazini na jimbo la Ituri kwa usafirishaji wa watu na bidhaa. Je, kuna matumaini yoyote kwa watumiaji wa barabara hii wakati msimu wa mvua tayari umekaribia na barabara inakarabatiwa kwa mikono? Ili kujadili hili, tunamkaribisha kama mgeni msimamizi wa kazi ya matengenezo kwenye mhimili huu wa barabara. Pharaon Tibasima anazungumza kwa simu na Marc Maro Fimbo.
/sites/default/files/2025-04/300425-p-s-invitebenipharaontibasimaroutebeni-kainama-00-web.mp3