Katika jiji la Beni, huko Kivu Kaskazini, polisi wa MONUSCO UNPOL, kwa ushirikiano na shirika la Tendo la Roho, waliandaa kikao cha uhamasishaji siku ya kwanza tarehe tano Mei, 2025, kwa wafanyakazi wa mtaa Beu. Miongoni mwa mada za kikao hiki cha kuongeza ufahamu: ujuzi juu ya mamlaka mpya ya MONUSCO, jukumu la polisi wa MONUSCO na polisi wa kitaifa wa Kongo, nguvu za kiume chanya, unyanyasaji wa kijinsia na mengine. Kwa nini ufahamu huu kwa wakati huu maalum? Tulizungumza kulihusu na afisa wa mawasiliano wa shirika la Tendo la Roho katika jiji la Beni. Ange Maliro akizungumza na Marc Maro Fimbo.
/sites/default/files/2025-05/280525-p-s-invitebeniangemalirochargeecommunicationtendolaroho-00.mp3