Habari za asubui, siku ya tano, 05 juni 2026

Waziri wa elimu ya kitaifa, Raisa malu, alizindua rasmi siku ya ine mjini Kinshasa Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi (ENAFEP). Waziri aliwaomba wanafuzni kuamini maarifa waliyopata shuleni ili kufaulu katika mtihani huu.

Zaidi ya watu mia moja waliuawa katika ajali za barabarani kwenye barabara kadhaa jimboni Haut-Katanga katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Tume ya Kitaifa ya Usalama Barabarani (CNPR) ya Haut-Katanga inayo toa habari ina endelea na juhudi zake ili kupunguza idadi ya ajali katika jimbo hilo.

Na huko Matadi, wasanii wanao tengeneza sanamu za mbao na vingine vifaa vya sanaa wana sema kwamba wanakosa wateja. Kwa maoni yao, moja ya sababu ya mateso yao ni imani fulani za kidini zinazohusisha sanamu za mbao, hasa zile za Kiafrika, na miungu.  

/sites/default/files/2026-06/05062026_-_jp_sw_-_matin.mp3