Journal Matin

Habari z'asubuhi 04 Februari, 2025

  • Goma: Shughuli za kijamii na kiuchumi zilianza tena hii siku ya kwanza lakini kwa woga mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini, wiki moja baada ya kuingiya kwa waasi wa M23 wakiungwa mkono na Rwanda, na mapigano kati yao na jeshi la Kongo 
  • Lubumbashi : Vijana wanane waliohusika katika kifo cha mwanahabari Patrick Adonis Numbi walihukumiwa kifo jana siku ya kwanza na Mahakama Kuu ya Lubumbashi
  • Mbuji-Mayi: Bei ya Mfuko wa mkaa imepanda mjini Mbuji Mayi huko Kasai Oriental tangu wiki tatu sasa. Imetoka franga elfu makumi mbili na tano hadi kati ya franga elfu makumi ine na elfu makumi ine na tano za Kongo./sites/default/files/2025-02/040225-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3