Habari za siku ya tano jioni tarehe 8/12/2023
- Kivu Kaskazini- Mpango wa kuondoka kwa wanajeshi wa EAC unaanza leo siku ya tano na utaendelea hadi tareha saba mewezi wa kwanza mwaka ujao.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, hali ni mbaya leo hii katika eneo la Kalonge-Bihambwe mtaani Masisi.
- Jimboni Tanganyika, usalama na utulivu huonekana katika mtaa wa Nyunzu, barabara zote sasa zinapitika na jamii zote zinaishi kwa maelewano.
- Za uchaguzi: Wagombea wengi kwa ubunge majimbo na kitaifa wanasema wanakabiliwa na matatizo makubwa yakufanya kampeni.
- Huko Kivu ya Kaskazini, jumuiya ya kiraia ya Beni ilizindua jana siku ya inne, mfululizo wa kampeni za uhamasishaji juu ya kuzuia na kupunguza vurugu wakati wa kipindi cha uchaguzi katika eneo la Beni-Butembo na Lubero.
- Kwa karibu wiki mbili, mafuriko yamekuwa yakiendelea katika maeneo kadhaa huko jimboni kubwa ya Equateur.
- Katika jimbo la Kwilu, usafiri unarudi tena kwenye sehemu ya barabara kati ya Batshamba kwenye kituo cha mia sita na makumi sita na mbili hadi Kakobola ikipitia mji wa Gungu, mji mkuu wa mtaa wa Gungu.
- Na katika jimbo la Kivu ya Kusini, ugonjwa ambao haujulikani umekuwa ukiangamiza wanyama wa kufugwa katika eneo la Idjwi kwa siku kadhaa./sites/default/files/2023-12/081223-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3