Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 11/12/2023
- Katika jimbo la Kivu Kaskazini, mji wa Goma pamoja na mji wa Sake, karibu kuatchanishwa kabisa mbali na barabara tatu muhimu za huduma za kilimo ambazo zinawaunganisha na eneo lote la Masisi.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, siku ya kwanza hii ni ya siku ya tatu ya utulivu kwenye maeneo yote ya vita katika mtaa wa Masisi.
- Kuondolewa kwa wanajeshi wa kikosi cha EAC-RF inchini Kongo , karibu wa askari mia kenda wa kikosi cha Burundi waliondoka Goma wikendi hii.
- "Heshima , uhuru na haki kwa wote". Hii ndiyo mada ya sherehe ya miaka makumi saba na tano na ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na Siku kuu ya Kimataifa ya Haki za Kibinadamu, siku ya kwanza hii , katika hoteli ya Pullman hapa mjini Kinshasa.
- Katika mji wa Beni, karibu wanawake makumi tano, wanachama wa vyama vya wanawake walizungumza siku ya kwanza hii juu ya taratibu zitakazowekwa ili kukabiliana na tatizo la unyanyasaji dhidi ya wanawake.
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini, zaidi ya visa elfu makumi inne na tatu vya surua vilihesabiwa kutoka mwezi wa kwanza hadi mwezi wa kumi na mbili mwaka huu katika maeneo makumi tatu inne ya afya.
- Dola za kimarekani bilioni mia tatu ndio fedhza ya kibajeti itakayokusanywa kwa kipindi cha miaka kumi ili kutekeleza mpango wa serikali ya Adolphe MUZITO endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri.
- Huko Kasai Oriental, kampeni ya uchaguzi inafanyika vizuri katika mji wa Mbuji Mayi. Tangu kuanza kwa shughuli hii, hakuna matukio makubwa yaliyotolewa.
- Kuhusu Biashara ya mafuta kwenye mpaka wa Kavimvira, katika mji wa Uvira, jimboni Kivu Kusini. Wafanyabiashara wadogo wa mipakani wa Kongo wanasema wamefurahishwa na shughuli hii na wanakaribisha ushirikiano wao na huduma za mpakani./sites/default/files/2023-12/111223-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3