Habari za siku ya inne jioni tarehe 11/07/2024
- Majeshi ya jamuhuri ya kidemokratia ya Kongo FARDC yanaishutumu Rwanda kwa kutokuheshimu mapatano ya kibinadamu yaliyotangazwa na Marekani.
- Mkuu makamu wa jeshi la FARDC anayesimamia ujasusi aliwasili siku ya inne hi huko mjini Beni jimboni Kivu ya Kaskazini, kwa ziara ya kazi.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, harakati ya wakimbizi wanaorejea katika vijiji vyao inazingatiwa katika mtaa wa Rutshuru.
- Katika jimbo la Ituri, kamati za wakimbizi zinashutumu kutokuadhibiwa kwa wahusika wa mauaji ya zaidi ya watu mia moja kwa zaidi ya mwaka mmoja katika maeneo ya Savo na Benza katika mtaa Djugu.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, mji wa Beni hauna maeneo ya umma wala vituo vya kuongoza watoto.
- Mwanamuziki Koffi Olomide alijielekeza siku ya inne hii kwa baraza kuu la viombo via habari CSAC.
- Usumbufu katika kanisa Kuu la Katoliki la Kinshasa. Shirika liitwao (ACKIN) linashutumu kile linachoeleza kuwa ni usimamizi mbaya unaofanywa na Kadinali Fridolin Ambango mkuu wa kanisa jimboni .
- Kanuni mpya seneti zilikubaliwa siku ya tatu .Ilikuwa wakati wa kikao cha mashauriano ambako maseneta makumi mnane waliohudhuria walichagua kanuni hizo.
- Huko Kivu ya Kusini, wahanga wa mafuriko katika eneo la Katashola katika mtaa wa Kalehe ambao walipoteza paa za makao yao pia wanakabiliwa na shida ya ukosefu wa chakula.
- Katika jimbo la Kasai Oriental: kusimamishwa siku ya tatu mjini Mbuji Mayi, kwa shughuli zote za ujenzi wa nyumba zilizofanywa kwenye eneo la Mitembela zinazoleta mzozo kwa miezi kadhaa kati ya Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Bakuanga MIBA na wanamemba wa Chama cha BURP./sites/default/files/2024-07/110724-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3