Habari za jioni 11 Februari, 2025
- Bunia : Watu karibu makumi tano na mbili walikufa, wengine wengi kujeruhiwa na nyumba kuchomwa moto usiku wa kuamkia hii siku ya pili katika shambulio jipya la wanamgambo wa CODECO katika maeneo ya Laudjo, Lindu na Lodja katika tabaka Djaiba huko Ituri
- Goma : Mjini Goma, shirika la Jeunes Ambassadeurs pour la Paix et le Développement, linatahadharisha kuhusu kuwepo kwa mabaki ya makombora ya vita katika jiji hilo baada ya mapigano ya hivi majuzi yaliyotikisa jiji hilo
- Kalemie : Serikali ya jimbo la Tanganyika imeimarisha udhibiti katika bandari ya Kalemie kufuatana na hali ya usalama inayoendelea katika majimbo jirani ya Kivu Kaskazini na Kusini/sites/default/files/2025-02/110225-p-sw-journalswahilisoir-00-web.mp3