habari zetu za Jumatatu tarehe 22 september .
- Mapambano yamezuka upya kati ya FARDC, inayoungwa mkono na wa Wazalendo, zidhi ya AFC/M23, inayoungwa mkono na Rwanda, Kaskazini na Kusini mwa Kivu. Kurejeshwa huku kwa vita kunaonekana wakati hali ya mvutano unazidi kuongezeka. Ni kupitiya shutuma za pande zote za ukiukaji wa usitishaji mapigano, ijapo mazungumzo yao huko Qatar yanazorota.
- Huko Kasayi shughuli za shule katika eneo la Mweka zilianza upya Jumatatu hii. Ni baada ya wiki kadhaa za kusimamishwa kuhusishwa na janga la virusi vya Ebola.
- Ugonjwa wa Mpox, surua, na kipindupindu kwa sasa ni janga linaloathiri jimbo la Lomami. Hali ya mlipuko ya magonjwa haya matatu ilitangazwa katika mkutano wa baraza la mawaziri la mkoa wa Ijumaa iliyopita. Mpox ndiyo inakuja mbele ikiwa na idadi kubwa ya visa ikifatiliwa na suruwa kwa watoto.
/sites/default/files/2025-09/22092025-journalswahilisoir-00web.mp3