Mtaani Lubero, Kivu Kaskazini, familia zaidi ya Elfu sita (6,000 ) za watu waliozihama makaji zao zafahidika na vifaa muhimu vya nyumbani toka shirika la Msalaba Mwekundu Croix rouge, kwa udhamini wa UNICEF.
Pa Mwene-Ditu, meya wa mji amewaamuru wanabiashara kuondoka kando ya mabarabara na kuhamia katika soko kuu la mji ili kupunguza ajali, msongamano na uchafu.
Na huko Matadi, watu sita wamefariki ndani ya muda wa chini ya wiki moja katika gereza la Boko, wilayani Mbanza-Ngungu. Chanzo cha vifo hivyo bado kulikana.
/sites/default/files/2026-08/10082026-journal_swahili_de_ce_lundi_matin_-00.mp3






