Journal Swahili Mercredi Matin, 12 aout 2026

Mjini Lubumbashi, watu 22 wamefariki katika ajali ya barabarani eneo la kuelekea Likasi. Hawa ni jumla ya abiria waliokua munamo basi dogo iliyohusishwa munamo adaji iyo, kwa mujibu wa Shirika la Kitaifa la kufwatilia Ajali za Barabarani, CNPR.

 Jimboni Ituri, Gavana hutoa wito kwa wanamgambo kuacha silaha. Jamadari Gaby Kasongo amesisitiza nia yake ya kurejesha amani katika eneo lote la Djugu na kuwataka wanamgambo kujitenga na makundi yenye silaha.

/sites/default/files/2026-08/120826-p-s-bloc_complet_journal-00.mp3