Habari za siku ya kwanza jioni
- Kumefunguliwa leo siku ya kwanza mjini Kinshasa mikutano kuhusu mazingira iitwao PRECOP 27.
- Mtu yeyote anayetaka kujenga lazima aulize mafundi wanaojulikana katika muundo unaosimamia masuala ya ujenzi ili kukabiliana na tukio lolote linalotokana na ujenzi usiyofaa .
- Katika jimbo la Ituri, watu kumi na wanne waliuawa na makao makumi matatu na sita kuunguzwa wakati wa shambulio la waaso wa ADF mwishoni mwa juma huko Kyamata katika usulutani wa Tchabi kusini mwa mtaa wa Irumu.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, raia kumi na mumoja waliuawa katika shambulio la waasi wa ADF jana siku ya mungu katika kijiji cha Beu Manyama, katika sekta ya Beni Mbau mtaani Beni.
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini, hali yaendela kuwa mbovu tangu usiku ya siku ya mungu huko Kamanyola, mtaani Walungu, kaskazini mwa eneo la Uvira.
- Jimboni Kongo Central, zaidi ya wakaadji makumi saba wa kijiji cha Kimbongo katika sekta ya Boko, mtaa wa Mbanza Ngungu, hawana tena mahali yakuishi
- Kasaï ya mashariki: barabara kuu mitatu ya mji wa Mbuji Mayi zitawekewa lami mwezi huu wa kumi kupitiya mradi wa Tshilejelu.
- Katika jimbo la Maniema, karibu mwezi mmoja baada ya kuanzishwa rasmi kwa shughuli ya kuhesabu wanafunzi wote na shule za kipekee , operesheni hii inaendela lakini kwa shida fulani kulingana na mkurugenzi jimboni wa offisi ya uchunguzu SECOPE./sites/default/files/2022-10/031022-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3