Habari za siku ya pili jioni
- Waziri wa Mazingira Eve Bazaiba anatangaza kwamba inchi ya Kongo ya Kidemokratisa inakuwa kwa sasa sawasawa na Indonesia na Brazili katika mkakati wa kugombea haki za wakaadji wake .
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, Prince Kihangi, mwanabunge jimboni anapendekeza mtaa wa walikale ushurutishwe na mradi wakupewa mkopo wa kaboni
- Katika jimbo la Kwilu,ma adui wawili wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya wakuu wa vijiji vya BUKUSU na FADIAKA, waliokamatwa walipelekwa siku ya kwanza mjini Bandundu.
- Katika jimbo la Kivu ya Kasakazin, Msemaji wa operesheni za kijeshi Sokola ya kwanza anatoa wito kwa wakaadji wa Butembo na eneo zima kuwa waangalifu ili kupambana na tishio la kigaidi
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini , kuliandaliwa siku ya pili hii siku bila kazi yoyote katika mtaa na mji wa Uvira na vile vile katika mji wa Sange.
- Katika jimbo la Maniema, kiongozi wa kabila ya BANGUBANGU LULINDI anayeishi mjini kindu anasema kwamba karibu vijiji kumi na kenda havina tena wakaadji wao
- Jimboni Tanganyika, meya wa mji wa Kalemie ametangaza siku ya pili hii kuwepo ugonjwa wa kipindupindu katika mji huo.
- Jimboni Kivu ya Kusini, kilalo cha muda cha Cihanda katika eneo la Nyangezi mtaani Kabare kilizinduliwa siku ya pili hii./sites/default/files/2022-10/041022-journalswahilisoirh00-00_web_0.mp3