Kituo cha afya cha Unité kilicho kaskazini mwa mji wa Butembo katika Kivu kaskazini kimerekodi ukosefu wa wagonjwa katika siku za hivi karibuni. Hali hii inatokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya makundi yenye silaha kwenye kambi ya jeshi iliyo karibu na kituo hiki cha afya, katika seli ya Mihake, manispa Bulengera. Kwa hivyo wasimamizi wa kituo hiki cha hospitali wanaomba viongozi wahamishe makao hayo ya jeshi ili kuwaepusha wakazi, hasa wagonjwa, kutokana na matokeo ya mashambulizi haya. Ili kulizungumzia, tunampokea Mumbere Vatsikirire Georges, Meneja Msimamizi wa Kituo cha afya cha Unité. Anazungumza na Grevisse Salumu./sites/default/files/2022-12/201222-p-s-butemboinviteagishopitalunite-00_web_.mp3