Karpate Tulinabo, Mratibu wa shirika ya haki za binadamu ADEC-DDH

Mwalikwa wetu ni Mratibu wa shirika lisilo la  kiserikali kwa maendeleo, elimu ya uraia na utetezi wa haki za binadamu, ADEC-DDH. Katika mahojiano na mwenzetu wa Goma   Gabriel Wamenya, muhusika  huyu wa masuala ya haki za binadamu, anazungumzia mikakati ya mawasiliano pamoja na matokeo yanayotarajiwa baada ya kuanzishwa wikendi iliyopita kwa kampeni ya uhamasishaji kuhusu  katiba ya Azimio la Kimataifa la Haki za binadamu. Kampeni hiyo inafanywa kwa ushirikiano na offisi ya BCNDH ya MONUSCO. Tumsikilize  KARPATE TULINABO katika  mazungumuzo  haya na  Gabriel Wamenya./sites/default/files/2023-05/130523_inviteswahili_web.mp3