Habari z'asubuhi 29 Mei, 2025
- Beni : Ni Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa, hii siku ya ine tarehe makumi mbili na tisa Mei. Katika hafla hii, liwali wa Kivu Kaskazini anatoa pongezi kwa walinda amani wa MONUSCO kwa jukumu lao katika harakati za kuleta utulivu mashariki mwa DRC
- Bunia : Mazungumzo kati ya jamii za wa Hema na wa Lendu yalianza hii Siku ya tatu tarehe makumi mbili na nane Mei huko Fataki katika tarafa la Djugu, jimboni Ituri. Lengo ni kupunguza mivutano kati yao
- Kinshasa : Mchakato wa kupata pasipoti mpya ya kibayometriki utaanza Siku ya ine tarehe tano Juni mwaka huu. Waziri wa Mambo ya Nje,Thérèse Kayikwamba Wagner, anasema kwamba kuzindua pasipoti hii mpya ni matarajio katika kukabiliana na mabadiliko ya viwango vya kimataifa./sites/default/files/2025-05/290525-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3