journal matin

Habari zetu za Jumatano tarehe 1 octoba 2025.

  • Kinshasa : Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, amehukumiwa kifo. Uamuzi huo ulitolewa Jumanne hii, Septemba 30, na Mahakama Kuu ya Kijeshi mjini Kinshasa, mshtakiwa akiwa hayupo.
  • Kinshasa : "Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasalia kuwa ahadi kwa kiasi kikubwa. Kuna tafauti kati ya maendeleo tunayoyaona kwenye karatasi na ukweli tunaouona ndani ya jamii, ambao unaendelea kukumbwa na ghasia." Hotuba ya Bi Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC na Mkuu wa MONUSCO.
  • Mbujimayi : Kasai Mashariki, habari njema kwa wanafunzi wa univasti katika eneo la Kasai Kubwa. Kazi ya ujenzi na uboreshaji wa Chuo Kikuu Rasmi cha Mbuji-Mayi imekamilika kikamilifu nakufurahisha wakaaji wote. Wawa walifanya safari ya kutembelea kituo hiki cha chuo kikuu.

/sites/default/files/2025-09/011025-p-s-journalswahilimatin-web.mp3