Habari za siku ya inne jioni tarehe 14/12/2023
- Siku chache kabla ya uchaguzi, mahitaji ya vieti via uchaguzi yamekuwa mengi huku huduma ya utoaji ni ngumu sana, wanalalamika baadhi ya wachaguzi ambao wakati mwingine hulazimika kusubiri kwa zaidi ya wiki moja ili kupata cheti hicho.
- Vietu vietu via uchaguzi viote havisomeki, na si mara zote tumeweza kupata vingine kutoka CENI. Tutafanya dje ili kuchaguwa wagombea wetu katika uchaguzi wa pamoja uliopangwa kufanyika tarehe makumi mbili mwezi huu?? Hivi ndivyo wanavyoshangaa wakazi kadhaa wa mji wa Bandundu katika jimbo la Kwilu.
- Jimboni Kivu ya Kusini, katibu mkuu jimboni ya CENI anahakikisha kuhusu maendeleo mazuri ya mchakato wa uchaguzi katika jimbo hilo.
- Katika jimbo la Tshopo, chini ya wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Kongo , kiongozi kuu ya CENI jimboni anasema tayari wamesambaza zaidi ya asilimia makumi kenda na tano ya vifaa vya uchaguzi katika eneo lote.
- Huko mjini Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini, kiwango cha kwenda mhali ya kula na kunywa yani baa kimeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi.
- Huko Ituri, kampeni ya uchaguzi ni ya kutisha sana katika usulutani wa Banyari Tchabi na maeneo mengine vingine jirani kusini mwa Irumu.
- Tume ya Maaskofu ya Haki na Amani ya Jimbo Kuu la Lubumbashi inafanya kampeni kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi wa amani.
- Katika jimbo Ituri, zaidi ya hekta elfu nne na mia tano za mazao ya mchele na mimeya mingine , viazi na mboga nyingine zimeharibiwa tangu siku ya pili na mafuriko ya Ziwa Albert katika mtaa wa Djugu.
- Huko Kivu ya Kaskazini, Kamanda wa Kikosi cha EAC anaelezea wasiwasi wake kuhusu usalama wa watu na mali katika maeneo ya Rutshuru, Nyiragongo na Masisi baada ya kuondolewa kwa askari wa kikosi hicho./sites/default/files/2023-12/141223-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3