Habari za siku ya inne jioni ya tarehe 15/06/2023
- Ni siku ya inne hii ndio mitihani ya Kitaifa la Uchaguzi, Mwelekeo wa Kielimu na Kitaalamu, TENASOSP ilianza .
- Huko jimboni Maniema, liwali wa muda AFANI IDRISSA MANGALA ndiye aliyezindua mitihani hii kutoka shule ya msingi kindu ville mbele ya viongozi kazaa wa jimbo hili.
- Katika jimbo la Equateur , liwali makamu na liwali wa muda alialika siku ya inne hii wanafunzi wenye kufanya mitihani wa kitaifa wa ya TENASOSP kukimbiza woga. Lakini kutumika kwa utulivu. Kwa hivyo, watafaulu katika mitihani hii .
- Kufuatana na kikao la kumi na nane la wiki ya madini ya Kongo yakidemokrasia, shirika la maendeleo la Marekani linasema liko tayari kusaidia Kongo kukuza sekta yake ya madini.
- Maendelo bora ya uvuvi yakudumu na ufugaji wa samaki ni shughuli muhimu kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi makumi mawili na mbili, wanamemba wa Mkutano wa Mawaziri wa Ushirikiano wa Uvuvi kati ya Nchi za Afrika zinazokuwa kando na Bahari ya Atlantiki .
- Katika jimbo la Ituri, zaidi ya visa elfu moja na mia tano vya surua vimeripotiwa katika muda wa miezi minne katika eneo la afya la Nia-nia, yapata kilomita mia tatu kutoka mji wa Bunia mtaani Mambasa.
- Jimboni Kivu ya Kusini, kampeni dhidi ya ugonjwa wa kiumbe cha kizazi ilizinduliwa siku ya tatu hii mjini Bukavu .
- Ujumbe wa viongozi wa wanamgambo maimai TWA wakiongozwa na mkuu wa kijiji Kasebu walikutana siku ya tatu hii huko Kalemie na waziri jimboni wa mambo ya ndani wa jimbo la Tanganyika./sites/default/files/2023-06/15062023-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3