Journal Soir

Habari za siku ya tatu jioni tarehe 30/11/2022

  • Maelfu ya vijana kutoka maeneo mbali mbali inchini Kongo walienda siku ya tatu hii kwenye ikulu ya wananchi kwa mkutano ulioitwa "Rais wa Jamhuri mbele ya vijana". Katika ukumbi wa mkutano wa Bunge la Kitaifa, Mkuu wa Nchi Félix Tshisekedi alipendekeza kwa vijana wa Kongo kushiriki kwa wingi katika chaguzi zijazo si tu kama wapiga kura bali kama wagombea ili kutoa upepo mpya katika changamoto nyingi za nchi.
  • Kazi halisi za awamu ya tatu ya mchakato wa kurejesha amani mashariki mwa DRC zimeanza siku ya tatu hii  asubuhi katika hoteli ya Safari Park jijini Nairobi.
  • Huko Kivu Kaskazini, licha ya wito wa kusitisha mapigano uliozinduliwa na Wakuu wa Nchi za EAC kwa ajili ya mchakato wa amani unaoendelea, makundi mengi yenye silaha yanahusika katika mapigano dhidi ya waasi wa M23.
  • Umakini ambao Rais wa Jamhuri aligusia wiki chache zilizopita katika hotuba yake kwa taifa hauko wakuchanganya na vyovyote vile na uundwaji wa makundi yenye silaha.
  • Huko Ituri, msimamizi wa kijeshi wa tarafa la Mambasa anakashifu uamuzi wa shirika la raia la eneo hili kusukuma wafanya biashara kutolipa ushuru katika eneo hili lote. 
  • Huko Kwilu, shirika la raia katika tarafa la Gungu linalaumu kesi za kujitendea haki zinazofanywa na raia katika eneo hili.
  • Katika mji wa zamani wa Kwilu Ngongo, katika tarafa la Mbanza Ngungu katika Kongo centrale, ugomvi uliotokea usiku wa hii siku ya pili kati ya makundi mawili ya mabandia ulisababisha uharibifu wa mali mengi.
  • Katika jimbo la Kasai-Oriental, tuzungumze kuhusu ugumu wa kuhifadhi miili ya wafu katika hospitali za jimbo hilo./sites/default/files/2022-11/30112022_-p-s-journalswahilisoir-_00_web.mp3