Habari za siku ya pili asubuhi
- Mjini Kinshasa, soko kuu la Shoprite GB litafunga milango yake tarehe makumi tatu mwezi wa kumi
- Jimboni Kasai-Oriental, wiki moja baada ya kuwashwa umeme jijini kwa saa chache, Mbuji-Mayi imerudi tena gizani.
- Kazi za ujenzi wa kilomita sita za barabara ya kitaifa namba mbili kati ya jiji la Bukavu na uwanja wa ndege wa Kavumu zinaendelea kawaida.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, operesheni ya lipiza ushuru kwa gari ilianza katika mji wa Goma hii siku ya kwanza.
- Katika mtaa wa Beni, msimamizi wa oparesheni za kudumisha na kurejesha utulivu wa umma kwa polisi wilayani alitangaza hii siku ya kwanza mbinu mpya ya operesheni za polisi, ile ya kufanya kazi na FARDC katika operesheni za pamoja kwa lengo la kuweka usalama katika miji iliyo chukuliwa na jeshi.
- Siku mbili baada ya kutoroka kwa karibu wafungwa mia mbili kutoka gereza kuu la Matadi, mfumo wa mashauriano wa mashirika ya kiraia wa Kongo Centrale unahofia kuzuka upya kwa ukosefu wa usalama.
- Jimboni Maniema, gereza kuu la Kasongo limerekodi tena kifo kingine kimoja wikendi hii. Kifo kilithibitishwa na mkurugenzi wa gereza hili.
- ''Fanya afya ya akili kwa wote kuwa kipaumbele cha kimataifa''. Hii ndiyo mada ya Siku ya Afya ya Akili Duniani mwaka huu inayoadhimishwa tarehe kumi mwezi wa kumi./sites/default/files/2022-10/11102022_-p-s-journalswahilimardimatin-00_web.mp3